JUACALI LYRICS

"Niimbie"
(feat. Enika)

Verse 1

Nani amekunoki zaidi kunishinda
Ukiniita kila siku naitika
Unakumbuka pahali nilikuona mara ya kwanza
Nilikua 5 yrs hapo kejani na brother
Nilikuchukua nikakuingiza kwa TAPE
Nikakuskizia nikasema hey
We ni noma naeza ka na wewe
Ebu songa  naeza cheza na wewe
Game yoyote utafkiria
Ukikatika me naku unganishia
Umepona sai jiskizie
Mashini ikisonga ebu niimbie

Chorus

Tulijikaza na mwishowe tukaweza
Tulisumbuka na mwishowe tukapenya
Popote tunaenda wote watupenda
Tulijikaza na mwishowe tukaweza

Verse 2

Sai umegeuka unaitwa L.P
Lazima nijichunge usinidunge na pini
Unaruka ruka na sijui ni kwa nini
Dawa yako nakushikilia na shilingi
Naona mbuyu siku hizi unambamba
Na lugha mpya ati inaitwa lingala
Kwa club nakuskuma hautoki
Ni saa kumi usiku bado hauchoki
Tuende mtaani tutulie
Stima ndio hio nikuandalie
Umenona sai jiskizie
Mashini ikisonga ebu niimbie

Chorus

Verse 3


Umependa video sana siku hizi
Kila mtu anaringa anakuita C.D
Naona umeoga  umepunguza uchafu
Dance basi mbele ya watu
Angalau tukuone
Ma pirates nao wasikuchome
Wanaku haribia biashara
Na kipindi ya sai nilala salama
Nakuingia unapumua reggae
Mtoi wetu wa kwanza ataitwa genge
Kenya mzima tunaifungua
Uganda na bongo tulishazichukua
Miaka tisa ni mingi sana
Waalike kwa harusi waambie tunaoana
Pete nazo tunavishana
Tuna hapa hatuta achana
Akili ni nywele kila mtu na yake
Mdomo ulimi na kupiga mate
Hii safari mpaka kilele
Sauti yangu nakupa milele
Naona beste yako RADIO  yuko hapa
T.V na ma PRESENTER wote
Waimbie basi

[www.mistari.com]
All lyrics are property and copyright of their owners. All lyrics provided for educational purposes only.
Copyright © mistari.com 2009