MBUVI LYRICS

"Nishike"

Adui wanizingira, rafiki kawa duni,
Mashaka kanipata, matata kawa mengi,
Maovu yamezidi, wema kadhulumiwa,
Nakulilia ee Bwana, ndiwe nategemea.

Nikilemewa nishike, nishike (nishike mkono Baba)

Nionyeshe njia yako baba x2

Nuru yangu na wokovu, sitaogopa kitu,
Ndiwe unipaye nguvu, na kuniweka huru ,
Wema wako na fadhili, zaniandama mie,
Mambo yakinizidi, ndiwe mwamba salama

Chorus

Nikilemewa nishike, nishike (nishike mkono Baba)
Nikilemewa nishike, nishike (nishike mkono Baba)
Nikilemewa nishike, nishike (nishike mkono Baba)
Nionyeshe njia yako Baba x4

Bridge

Kando ya maji matulivu wewe waniongoza,
Waniandalia karamu, mbele ya adui zangu.

Nishike, (nishike mkono Baba), nishike, (nishike mkono Baba)

Njia yako Baba x2

Chorus

Nikilemewa nishike, nishike (nishike mkono Baba),

Nionyeshe njia yako Baba x2

[www.mistari.com]
All lyrics are property and copyright of their owners. All lyrics provided for educational purposes only.
Copyright © mistari.com 2009